Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amewapongeza watu wa Nepal kwa uchaguzi wa bunge:

Ban amewapongeza watu wa Nepal kwa uchaguzi wa bunge:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa Nepal kwa kuendesha uchaguzi wa bunge kwa amani na mafanikio.

Amesema Idadi ya watu waliojitokeza inadhihirisha nia yao ya kusukuma mbele mchakato wa amani.

Bunge hilo jipya litakuwa na majukumu ya kihistoria ya kukamilisha katiba mpya, kuendeleza mafanikio ya mchakato wa amani yaliyopatikana hadi sasa na kuchagiza majadiliano ya kitaifa na maridhiano.

Ban amesema Umoja wa mataifa bado utaendelea kuisaidia Nepal katika hatua ya mpito kuelekea muskhabali wa amani, demokrasia na matumaini.