Fedha ni muhimu kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi: Ban

20 Novemba 2013

Mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea huko Warsaw Poland umeingia siku ya pili ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema uchangishaji fedha kwa ajili ya harakati za kupambana na mabadiliko hayo ni suala muhimu. Akizungumza kwenye kikao cha mawaziri, Ban amesema jambo muhimu kwanza ni sera bora za uwekezaji usioharibu mazingira lakini utoa ajira na mifumo ya udhibiti wa uharibifu wa mazingira lakini jambo la pili na tatu ni fedha kutoka sekta ya umma, sekta binafsi na mfuko maalum wa kusaidia mipango hiyo kwani mabadiliko ya tabianchi ni tishio.

(Sauti ya Ban)

"Mabadiliko ya tabianchi ni tishio kwa uchumi wa nchi maskini na tajiri na kwa utulivu wa mfumo wa fedha duniani. Kadri tuchelewavyo, gharama nazo zaongezeka kwa jamii, kwa uchumi wetu na kwa sayari yetu.”