Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani vikali shambulio la Beledweyne Somalia:

Ban alaani vikali shambulio la Beledweyne Somalia:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio lililokatili maisha ya watu dhidi ya kituo cha polisi huko Beledweyne, Somalia,. Shambulio hilo limefuatia mashambulio mengine kadhaa kama hayo katika wiki za hivi karibuni. Ban amesema vitendo hivyo vya kigaidi dhidi ya serikali na watu wa Somalia vimesababisha machungu makubwa.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na kwa waliojeruhiwa. Pia amepongeza vikosi hususani vya polisi ambavyo kwa ujasiri wao walifanikiwa kuwafurusha washambuliaji hao.

Ameongeza kuwa amejizatiti kuisaidia serikali ya Somalia kuzuia mashambulizi kama hayo na kuliweka taifa hilo katika njia ya kuelekea amani na usalama. amerejea kusisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia serikali ya Somalia, taasisi zake na watu wa nchi hiyo ili kufikia azma ya amani.