Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika hatarini kuingia kwenye gharama kubwa –UNEP

Afrika hatarini kuingia kwenye gharama kubwa –UNEP

 Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP imesema kuwa gharama ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika itaongezeka kwa kiasi kikubwa iwapo hatua mahsusi hazitachukuliwa hivi sasa. Yakadiriwa kwamba Afrika inaweza ikaingia gharama ya dola Bilioni 350 kila mwaka ifikapo mwaka 2070 iwapo wakati huu itashindwa kutekeleza mipango ya kupunguza athari za uharibifu wa mazingira.Gharama hiyo itajitokeza iwapo kiwango cha nyuzi joto cha sasa ambacho ni Mbili kitaongezeka. UNEP inasema iwapo bara la Afrika litachukua hatua sasa gharama zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi zinaweza kupungua hadi kufikia bilioni 150 kwa mwaka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo mjiniWarsaw, Waziri waTanzaniaanayehusika na Mazingirawa Tanzania Dr.Terezya Huviza amesema Afrika haiwezi kucheza mchezo hatari wa kupuuzia kutekeleza majukumu yake hasa wakati huu ambapo idadi ya watu inaendelea kuongezeka na kufikia bilioni 2 mwaka 2050.

Amesema nchi za Afrika zimedhamiria kutekeleza mipango itakayowezesha kukabiliana na suala tete la mabadiliko ya tabianchi.