Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji zaidi ya milioni tano wanaishi Italy: IOM

Wahamiaji zaidi ya milioni tano wanaishi Italy: IOM

Ripoti ya kuhusu uhamiaji iliyozinduliwa na ofisi ya taifa ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Italia na taasisi ifahamikayo kwa jina la IDOS inaonyesha kuwa nchi hiyo ina wahamiaji zaidi ya milioni tano ambayo ni asilimia 7.4 ya idadi ya watu. Ripoti hiyo kadhalika inabainisha kuwa wahamiaji nchini Italia wanachangia asilimia 12 ya pato la taifa na kulipa kodi ya euro billion 13.3 kwa mwaka. Hii ina maana gani? Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM .

 (SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)