Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCRM yatilia shaka baada ya kuzuka upya machafuko Libya

OHCRM yatilia shaka baada ya kuzuka upya machafuko Libya

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani na kuelezea masikitiko yake kutokana na kujirudia upya machafuko nchini Libya ambayo yamesababisha zaidi ya watu 40 kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa tangu yaliyozuka ijumaa iliyopita. Grace Kaneiya na maelezo kamili

 (RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Kumekuwa na ongezeko kubwa la umwagaji damu katika mji mkuu wa Tripoli tangu kumalizika kwa machafuko mwaka 2011. Katika siku za hivi karibuni hali ya wasiwasi imeongezeka kutokana na kujitokeza kwa matukio ya utekaji nyara na mashambulizi ya kushtukiza.

Ikielezea hali hiyo, Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa kile kinachoshuhudiwa sasa nchiniLibyahakiwezi kuvumilika na imezitaka mamlaka za dola kujiepusha na matumizi ya nguvu kudhibiti makundi ya watu wanaoendesha maandamano ya amani. Ravina Shamdasani ni afisa wa ofisi ya haki za binadamu.

 (CLIP YA RAVINA SHAMDASANI)