Leo ni siku ya choo duniani:UM

19 Novemba 2013

Leo ni siku ya choo duniani inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa huku kukitolewa wito wa kuboresha mazingira na kuzingatia usafi wa vyoo vyenyewe. George Njogopa na taarifa zaidi

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Siku hii ya choo duniani inakumbusha ulimwengu kuwa watu zaidi ya bilioni 2.5 duniani kote wanakabiliwa na matatizo yanayoambatana na ukosefu wa vyoo vinavyokithi mahitaji ya wakati hatua ambayo inawaweka kwenye mazingira ya kukumbwa na matatizo ya kiafya.

Ripoti moja iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuambatana na siku hii inawataja wanawake na wasichana kuwa ndiyo walioko kwenye kundi hatarishi la kukubwa na matatizo ya kiafya na inataka kuwekwa msukumo wa kubadili hali hiyo

Ripoti hiyo imebainisha kuwa kila kwenye wanawake watata, basi mmoja amekumbwa na matukio ya kama vile yanayodharirisha utu wake,kunyanyasika hata kushambuliwa kutokana na kukosa sehemu salama ya kupata choo.

Inasadikika kuwa, zaidi ya wanake milioni 526 duniani kote wanakosa faragha ya kwenda kijisaidia hatua inayowalazimu kwenda maeneo ya wazi kwa ajili ya kupata choo.

Dr. Christopher Williams ni Mkuu wa baraza la maji na ushirikinano wa masuala ya usafi wa Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA DR CHRISTOPHER WILLIAM)