Familia nyingi Tacloban zimepoteza kila kitu:UNICEF.

19 Novemba 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema uharibifu uliosababishwa na kimbunga Haiyan mjini Tacloban na voinga vyake ni mkubwa saana.

Linasema familia nyingi zimepoteza kila kitu na msaada ndio unaanza kuwafikia huku serikali na mashirika ya makanisa yakiendelea kuwasaidia. Kwa mujibu wa UNICEF msaada wa haraka unahitajika ili kuzuia kusambaa kwa magonjwa na hasa maji yanahitajika haraka saana.

Jumatatu ijayo UNICEF na washirika wake wataanza chanjo ya surua na polio kwa watoto na pia kutoa kituo cha kuhifadhi chanjo, kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya watoto na kutoa msaada kwa watoto ambao wamepoteza wazazi wao na familia zao.