Filamu ya Mary na Martha yatanabaisha athari za malaria

19 Novemba 2013

Mpango wa kimataifa wa kudhibiti malaria,The Roll Back Malaria umeshirikiana na Richard Curtis ambaye ametengeneza filamu iitwayo Mary and Martha inayojikita katika kutanabaisha mkasa wa gonjwa la malaria.

Mada kuu ya filamu hiyo ni safari ya mama hao wawili mmoja toka Marekani na mwingine uingereza na kila mmoja wao ameathirika na malaria na maisha yao yanaungana kwa nia ya kupambana na gonjwa hilo katika nchi zao na kwingine duniani. Filamu hiyo imepata ushirikiano na msaada kutoka Roll Back malaria na inatumika kuelimisha kuhusu gonjwa la malaria kama anavyofafanua Richard Curtis

(SAUTI YA RICHARD CURTIS)

Ameongeza kuwa malaria ni ugonjwa hatari na ni janga lakini suluhu yake ni rahisi na ya gharama nafuu.

(SAUTI YA RICHARD CURTIS)