Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ayapongeza mataifa ya Baltic kwa kuwawezesha wanawake:

Ban ayapongeza mataifa ya Baltic kwa kuwawezesha wanawake:

Mataifa ya Baltic yamepongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa hatua waliyopiga katika kutumia teknolojia kwa ajili ya maendeleo na kuwawezesha wanawake.

Ban Ki-moon ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari Vilnius, mji mkuu wa Lithuania, wakati akihitimisha ziara yake ya mataifa ya Baltic Jumatatu. Amesema amehamasishwa saana na ari ya mataifa hayo katika kuendeleza demokrasia, haki za binadamu na maendeleo endelevu.

Ameongeza kuwa mataifa ya Baltic ni madogo lakini yana mchango mkubwa katika siasa za kimataifa, maendeleo na haki za binadamu.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

"Nchi za Baltic zinaonyesha jinsi ya kutumia teknolojia kwa maendeleo. Na naupongeza ukanda huu na viongozi wake kwa kushirikiana uzowefu wao wa teknolojia na nchi nyingine. Ziara yangu pia ilimulika uwezeshaji wa wanawake, suala ambalo nimekuwa nikiligusia kila wakati na viongozi hao. Katika nchi za Baltic countries,nimetiwa moyo na hatua walizopiga katika kuleta usawa hasa katika maisha ya kisiasa”

Ban Ki-moon ambaye pia alizuru Latvia na Estonia ameelekea Poland.