Spika Makinda asema mabadiliko ya sheria ya ndoa yana mlolongo mrefu

18 Novemba 2013

Mkutano wa nane uliwaokutanisha maspika wanawake duniani umemalizika mwishoni mwa juma mjini New York huku mjadala mkubwa ukiwa ni mkakati wa usawa wa kijinsia kuwa sehemu ya malengo endelevu ya milenia baada ya 2015.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Joseph Msami amekutana na kufanya mahojiano na miongoni mwa waliotoa mada katika mkutano huo, spika wa kwanza mwanamke nchini Tanzania Anna Makinda ambaye pamoja na mambo mengine anasema anazungumzia suala la mabadiliko ya sheria ya ndoa nchini humo inayoruhusu msichana mwenye umri wa miaka 18 kuolewa.Spika anasema mlolongo wa mabadiliko ni mrefu kulikoni? Kwanza Makinda anaanza kwa kueleza mjadala mkuu wa mkutano huo.

(SAUTI SPIKA-MAHOJIANO)