Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma ya maji yarejea huko Tacloban

Huduma ya maji yarejea huko Tacloban

Bado twaangazia kimbunga Haiyan ambapo hatimaye huduma kamili ya maji safi na salama imerejea kwa takribani watu laki mbili walioathriwa na kimbunga hicho kwenye mji wa Tacloban nchini Ufilipino na wilaya nyingine sita zinazozunguka mji huo. Kurejea kwa huduma hiyo kunafuatia kukamilika Jumapili usiku kwa ukarabati wa mtambo wa kutakasa maji. George njogopa na ripoti kamili.

(Taarifa ya George)

Tangu kuzuka kwa kimbunga hicho wiki moja iliyopita,mtambo huo wa uzalishaji maji ilikuwa ukizalisha chini ya kiwango na hivyo kuwafanya mamia ya manusura kuwa hatarini kukumbwa na magonjwa.

Juhudi kubwa zilichochukuliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la watoto UNICEF na lile la Marekani USAID imewezesha mtambo huo kupata mafuta na hivyo kurejesha uzalishaji wake katika hali ya kawaida.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Ufilipino Tomoo Hozumi ameelezea uwezekano wa kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko iwapo kutakosekana juhudi ya kusambaza maji salama. Amesema ili kukabiliana na hali hiyo kunahiutajika kusambazwa kiasi cha lita 15 za maji safi kila siku kwa familia zilizoko kwenye maeneo yaliyoathirika.