Wahudumu wa Afya wametia nanga Ufilipino: WHO

18 Novemba 2013

Nchini Ufilipino zaidi ya wiki moja baada ya kimbunga Haiyan kupiga eneo hilo, Shirika la afya duniani WHO linasema timu ya wataalamu wa afya inayofuatilia magonjwa iko nchini humo ijapokuwa hakuna mlipuko wa magonjwa uliokwisharipotiwa. Jason Nyakundi na Ripoti kamili.

(Ripoti ya Jason)

Mengi ya makao 1500 kwenye maeneo yaliyokumbwa na kimbuga yana misongamano ya watu na kuna hofu kuwa huenda kukatokea mikurupuko ya magonjwa.

WHO inasema kuwa usambazaji wa madawa unaendelea lakini bidhaa zaidi zinahitajika. Idara ya afya nchini Ufilipino inaendesha kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Surua na Polio kwenye maeneo yaliyoathirika.

Msemaji wa WHO Tarik Jasarevice ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa WHO inasaidia kurejesha huduma za vituo vya afya kwenye sehemu zizizoathiriwa.

(Sauti ya Tarik)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter