Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwepo na ushirika wa kiuchumi kuongeza uwekezaji OIC:UNCTAD

Kuwepo na ushirika wa kiuchumi kuongeza uwekezaji OIC:UNCTAD

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo na biashara UNCTAD kuhusu muundo wa uwekezaji wa kimataifa inasema uwekezaji wa moja kwa moja wa nje FDI kwenda kwa shirika la jumuiya ya ushirikiano wa n hi za Kiislam OIC umejikita katika baadhi ya nchi tuu.

UNCTAD inasema kwa kufanya hivyo umesalia kuwa mdogo katika uchumi wa shehemu hiyo tuu ikilinganishwa na makundi mengine ya mataifa yanayoendelea.

UNCTAD imependekeza kuwepo na ushirikiano wa kina na wenye wigo mpana zaidi miongoni mwa nchi za kanda ya OIC. Kwa mujibu wa ripoto ushirikiano huo utaunda masoko makubwa, kuwepo na shughuli na bidhaa maalumu na hivyo kuboresha na kuinua kiwango cha uwekezaji wa moja kwa moja toka nje.