Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa WFP akutana na manusura wa kimbunga Hyan mjini Tacloban

Mkuu wa WFP akutana na manusura wa kimbunga Hyan mjini Tacloban

Ingawa changamoto ya utaratibu wa ugavi inaendelea lakini chakula kingi kinaendelea  kuwasili Ufilipino nchi ambayo ilikumbwa na kimbunga Haiyan, kwa mujibu wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP.

Shirika hilolinasema chakula kwa watu zaidi ya laki saba kimepelekwa katika jamii zilizoathirika ikiwemo vifurushi vya chakulakamamchele na biskuti zenye kiwango cha juu cha nguvu mwilini.

 Mkurugenzi Mkuu wa WFP Ertharin Cousin ambaye amewasili katika mji uitwao Tacloban jumapili amekutana na manusura na maafisa wa serikali.

 Bi Cousin amesifu raia wa eneo hilo wanaofanya kazi na mashirika ya  Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada kwa namna walivyokabiliana na janga la kimbunga.

Mkuu huyo wa WFP anatarajiwa kutembelea kisiwa kiitwacho Payan jumatatu ambako WFP inaanzisha kituo cha kuhifadhi vifaa.