Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha hitimisho la uchaguzi wa rais nchini Maldives

Ban akaribisha hitimisho la uchaguzi wa rais nchini Maldives

Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidi mchakato wa kidemokrasia na mafanikio nchini Maldives , amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Kin Moon wakati akipokea hitimisho la kurudiwa kwa uchaguzi wa rais nchini humo.

 Katika taarifa uiliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu Jumapili, Bwana Ban amesema  kwa mara nyingine idadi kubwa ya watu waMaldiveswamejitokeza kupiga kura wakionyesha nia ya kumchagua rais ajaye, licha ya vikwazo na uchelewashaji.

 Katika uchaguzi huo Abdulla Yameen na rais mstaafu Mohamed Nasheed walikuwa wanagombea nafasi hiyo ambayo ililazimu uchaguzi kurudiwa mara tatu. Bwana Yameen  aliapishwa kuwa raisi jumapili baada kupata zaidi ya nusu ya kura.

 Bwana Ban amesema ushindani mkubwa uliojitokeza  unaonyesha haja kwa utawala mpya kuwahusisha wapinzani katika ujenzi wa taifa na kuongoza nchi kwa maslahi ya raia wote wa Malidives.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa tathimini ya awali ya waaangalizi wa kimataifa na wa ndani  inaonyesha kuwa uchaguzi umeendeshwa katika uwazi na kitaalamu.