Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanariwaya nguli Chinua Achebe aenziwa Umoja wa Mataifa:

Mwanariwaya nguli Chinua Achebe aenziwa Umoja wa Mataifa:

Hapa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa kumefanyika kumbukumbu maalum ya kumuenzi jabali wa fasihi na mwanariwaya nguli Chinua Achebe. Chinua Achebe aliyezaliwa tarehe 16 Novemba mwaka 1930 nchini Nigeria ni mashuhuri kwa kazi zake za fasihi ikiwemo riwaya kama ile ya “Things Fall Aparty” na mashairi. Vitabu vya Achebe vimevuka mipaka ya Nigeria, na hata bara Afrika na vinasomwa mabara mengine jambo ambalo Olutosin Mustapha mwalimu katika shule moja Brooklyn mjini New York, Marekani na pia mchapishaji anajivunia.

Ninafurahia sana pindi nikienda shule na kupata kwamba wanafunzi wanasoma  kitabu cha Things fall apart kwa sababu kitabu hiki nilikisoma kama msichana mdogo nchini Nigeria lakini sikukielewa hadi nilipofika chuo kikuu. Cha kustaajabisha kwangu ilikuwa nilipofika hapa Marekani nikiwa mwalimu mbadala nikifundisha shule mbali mbali niliona kwamba wanafunzi walikuwa wanasoma kitabu cha Things Fall apart ni kitabu kizuri sana cha fasihi na mwaka ulipoita katika shule ninakofundisha kuna mtoto ambaye alipata asilimia 100 kwa mia katika fasihi.”

Kwa upande wake Abena Busia ambaye ni Profesa wa Kiingereza katika chuo kikuu cha Rutgers nchini Marekani ambaye alihudhuria Sherehe hiyo alisema alipata fursa ya kukutana na Chinua Achebe na kitu anachokumbuka sana ..

“Wakati wa furaha sana kwangu ilikuwa siku moja 2008 katika mkutano wa siku mbili wakusherehekea kuchapishwa kwa kitabu cha Things fall apart nilipata fursa katika kilele cha mkutano huo kusoma shairi wakati Achebe akielekea kwenye jukwaa.”

Chinua Achebe alifariki dunia mwaka huu mwezi Machi mwaka huu wa 2013 nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 82.