Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la kuahirisha kesi ya viongozi wa Kenya ICC halijaenda kombo: Balozi Macharia

Suala la kuahirisha kesi ya viongozi wa Kenya ICC halijaenda kombo: Balozi Macharia

Mwakilishi wa kudumu wa KenyaKwenye Umoja wa Mataifa Balozi Macharia Kamau akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi tu baada ya Baraza la Usalama kukataa rasimu ya azimio la kuahirisha hadi wakati muafaka kesi zinazokabili viongozi waandamizi wa Kenyakwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague. Balozi Kamau amesema kilichojiri kwenye upigaji kura ni masikitiko makubwa lakini kimefungua mwanga kwa bara la Afrika kwani kimedhihirisha mshikamano wa kipekee kwa mshikamano wa Afrika na kubadili kabisa bila shaka yoyote masharti ya ushirikiano wa Afrika na jumuiya ya kimataifa kuanzia leo.    Balozi Kamau akawaeleza waandishi kuwa wana uhakika malengo ambayo Afrika ingetaka kuona yanakamilika basi katika siku na wiki zijazo bila shaka yatafanya hivyo na hapa akafunguka zaidi alipohojiwa na Joseph Msami wa Idhaa hii.

 (Sauti ya Balozi Kamau)

 Mwakilishi wa Kundi la Afrika Balozi Tekeda Alemu kutokaEthiopia, amesema ni lazima sasa Jumuiya kimataifa ikafahamu kuwa hoja ya suala la Kenya ICC kuahirishwa siyo tena yaKenyapekee bali ni ya Afrika na kwamba kilichojiri si uhalisia.

 (Sauti ya Balozi Alemu)

 “Kilikuwa ni kikao cha kuvunja moyo bila shaka. Lakini kwa upande mwingine tunahisi ni ushindi wa kimaadili kwa Afrika. Na msingi wa yote haya ni kwamba pengine hili ni suala la Kenya! Hili siyo suala la Kenya tena ni suala la Afrika.”

 Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Balozi Liu Jieyi akasema ni masikitiko kuwa azimio halikupitishwa ingawa lilikidhi ibara ya Sita ya mkataba wa Roma ulioanzisha ICC na matumaini yake ni kwamba hatua ya leo  haitaathiri uhusiano kati ya baraza lake na Muungano wa Afrika.