Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNECE yataka hatua kuchukukuliwa ulimwengu unapoadhimisha siku ya choo duniani

UNECE yataka hatua kuchukukuliwa ulimwengu unapoadhimisha siku ya choo duniani

Huku watu watu bilioni sita kati ya watu bilioni saba duniani kwa sasa wakiwa wanamiliki simu za mkononi ni watu bilioni 4.5 tu walio na choo, watu bilioni 2.5 wakiwa hana choo za kisasa huku watu wengine bilioni moja wakiwa hawa choo kabisa kwa mjibu wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya UNECE.

Kutokana na hili Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitenga tarehe 19 mwezi Novemba kila mwaka kuwa siku ya choo duniani. Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinatakiwa kubuni sera za kuhakikisha kuwepo kwa choo na usafi. Kuzuia watu kwenda haja kubwa maeneo yaliyo nje kutapunguza magonjwa ya kuendesha kwa asilimia 35 magonjwa yanayochangia vifo 750,000 vya watoto walio chini ya miaka mitano kila mwaka.