Ofisi ya haki za binadamu yalaani ubaguzi dhidi ya waziri wa sheria wa Ufaransa:

15 Novemba 2013

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo mashambulizi hayo ya wiki chache zilizopita yanajumuisha habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la kila wiki lililotoka Jumatano likiambatanisha picha yake na kichwa cha habari “hila kama tumbuli, Taubira arejeshewa ndizi” .

Ofisi ya haki za binadamu inasema azima ya ubaguzi wa rangi katika habari hiyo uko dhahiri, licha ya gazeti hilo kupinga shutma na kusema walikuwa tuu wanatumia misemo miwili ya Kifaransa ambayo hutumika saana na ambayo hutumika kumuelezea mtu ambaye anafuraha saana.

Tukio hili ni miongoni mwa mfululizo wa matukio kama hayo yanayomlenga Bi Taubira. Mwezi uliopita mmoja wa wagombea alimlinganisha waziri Taubira na nyani kwenye filamu fupi iliyorushwa hewani Oktoba 17.