Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakataa ombi la Kenya la kutaka kesi ziahirishwe

Baraza la Usalama lakataa ombi la Kenya la kutaka kesi ziahirishwe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo baada ya kupokea ombi kutoka Umoja wa Afrika la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi ya viongozi wa Kenya iliyoko Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC imepiga kura na kupinga ombi hilo. Flora Nducha na ripoti kamili.

 (Ripoti ya Flora)

 Ijumaa asubuhi wajumbe wa Baraza la Usalama walipokea ombi kutokaKenyana Muungano wa Afrika zikitaka kesi kesi dhidi ya viongozi waKenyaakiwemo Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto zisitishwe na ziahirishwe hadi muda muafaka.

 Sababu kuu zilizotajwa ni pamoja na kutoa fursa kwa viongozi hao kutekeleza azma yao ya kudhibiti vitisho vya kigaidi kama ilivyojidhihirisha kwenye shambulio la kigaidi mwezi Septemba na kuendeleza harakati za maridhiano kwani kufanyika kwa kesi sambamba na jitihada hizo kunaweza kutoa fursa kwa kuimarika kwa vitisho vya amani na usalama nchini humo na eneo la Mashariki mwa Afrika.

 Wajumbe 15 wanachama wa Baraza hilo la usalama walipiga kura ambapo Saba walisema Ndio na Wanane hawakuonyesha msimamo wowote huku hakuna mjumbe yeyote aliyepiga kura kusema HAPANA na hivyo Rais wa Baraza hilo akatangaza kutopitishwa kwa azimio hilo juu ya suala la Kenya huko ICC.

 (SAUTI YA BALOZI )                                  

 “Matokeo ya Kura ni kwamba Saba wameunga mkoni, hakuna aliyesema Hapana, na Wanane hawajasema chochote. Kwa hiyo azimio halijapitishwa kwa kuwa limekosa idadi ya kura zinazotakiwa kulipitisha.”

 Nchi ambazo hazikuonyesha msimamo ni pamoja na Guatemala, Luxemborg naArgentinaambazo katika mawasilisho yaobaada ya kupiga kura wamesema wanaamini kuwa ICC  imeanzishwa kwa ajili ya kuepuka watu kukwepa mkono wa sheria na kwamba hofu yaKenyainaweza kushughulikiwa kwa njia nyingine.