Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wanaojaribu kuingia Ulaya wakataliwa na kurejeshwa walikotoka:UNHCR

Wakimbizi wanaojaribu kuingia Ulaya wakataliwa na kurejeshwa walikotoka:UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema linatiwa hofu na hatua ya baadhi ya nchi za muungano wa Ulaya kuweka vikwazo vya kuingia au kuwarejesha kwa nguvu watu wanaoomba hifadhi wakiwemo wale waliokimbia machafuko nchini Syria.

Kwa mujibu wa shirika hilo Bulgaria mwishoni mwa wiki iliwakatalia kuingia wakimbizi 100 na kuweka polisi 1200 mpakani kudhibiti wakimbizi hao , wakati Ugiriki na Cyprus wakilaumiwa kutekeleza pia hatua hizo.

Uturuki kwa sasa ndiyo yenye idadi kubwa ya wakimbizi wa Syria wakiwemo 500,000 walioorodheshwa. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

UNHCR inatoa wito wa kimataifa ikiwemo kwa Muungano wa Ulaya kubadili mtazamo kutoka kulinda mipaka na kuanza kulinda watu.