Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya UNHCR kwa waathirika wa kimbunga Philippine yaanza kuwasili

Misaada ya UNHCR kwa waathirika wa kimbunga Philippine yaanza kuwasili

Kumekuwa na ongezeko kubwa la misaada kwa waathirika wa kimbunga Haiyan kilichowakumba raia wa Ufilipino baada ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR kusambaza misaada kadhaa kwa njia ya ndege.

Ndege mbili za shirika hilo zimekuwa zikidondosha misaada eneo Cebu ambalo limeaathiriwa zaidi na juhudi za kuyafikia maeneo mengine ikiwemo mji wa Tacloban zinaendelea kufanywa.

Kunataarifa pia misaada mingine kutoka Dubai inatazamiwa kuwasili kwenye eneo hilo wakati wowote kuanzia sasa.

Maafisa wa UNHCR wamesema kuwa misaada hiyo inayosambazwa imetolewa katika baadhi ya hifadhi yake ikiwemo pia kwa nchi washirika.Hadi sasa kiasi cha watu 7000 wamefikiwa na misaada mbalimbali.

Hali jumla katika eneo la Tacloban imeendelea kuwa mbaya kukishuhudiwa pia ukoserfu wa mahitaji muhimu.