Heko Afrika kwa kuchukua hatua kulinda albino: Ofisi ya Haki za binadamu

15 Novemba 2013

Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imepongeza hatua ya Tume ya Afrika ya kuridhia azimio la kwanza la ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi barani humo au Albino huku ikisema kilichobakia sasa ni utekelezaji na elimu kwa umma juu ya haki za msingi za kundi hilo. Msemaji wa Ofis hiyo Rupert Colville ameeleza kuwa utekelezaji ni muhimu kwani hadi sasa wanapokea ripoti za vitisho, ubaguzi na hata manyanyaso dhidi ya albino.

(Sauti ya Colville)

“Bado tuna hofu kutokana na vitisho wanavyopata albino. Twazisihi nchi zote za Afriak kutekeleza kwa dhati azimio hilo lililoridhiwa na tume ya Afrika na kuchukua hatua mahsusi kulinda haki ya kuishi na ulinzi ya albino.”

Azimio hilo limepitishwa tarehe Mosi mwezi huu muda mfupi tu baada ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la pili kuhusu albino mwezi Septemba.