Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo ya Malaria sasa majaliwa 2030: WHO

Chanjo ya Malaria sasa majaliwa 2030: WHO

Shirika la Afya duniani, WHO limetangaza lengo la kuwa na leseni ya chanjo dhidi ya Malaria ifikapo mwaka 2030. Imesema chanjo hiyo itakuwa na uwezo wa kupunguza wagonjwa wa Malaria kwa asilimia 75 na kutokomeza kabisa ugonjwa huo.  Taarifa zaidi na Flora Nducha.

 (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Mkurugenzi anayehusika na  mpango wa ugonjwa wa Malaria kwenye shirika la afya duniani WHO anasema kuwa dawa zilizo salama na za gharama ya chini zitakuwa na mchango mkubwa katika kuangamiza ugonjwa wa Malaria. Amesema kuwa hata baada ya kupigwa  hatua na uvumbuzi wa juu bado ghjarama ya ugonjwa wa Malaria ni kubwa.

Makadirio ya hivi majuzi  yaliyofanywa na shirika la afya duniani yanaonyesha kuwa ugonjwa wa Malaria unasababisha vifo 660,000 kila mwaka miongozi wa wagonjwa 219,000. Madawa mapya ni  lazima yawe na uwezo wa kutibu ugonjwa wa Malaria kwa asilimia 75 na yaweze kutimiwa kwenye maeneo yaliyo na visa vingi zaidi vya ugonjwa huo na pia yapate kibali cha kutumika ifikapo mwaka 2030.