Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wametelekezwa: Mia Farrow

Raia huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wametelekezwa: Mia Farrow

Jamhuri ya Afrika ya Kati  balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Mia Farrow ametaka hatua za haraka kumaliza ghasia nchini humo kwani raia ndio wanaoteseka na yaonekana wametelekezwa. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(Ripoti ya Jason)

Akizungumza baada ya ziara ya juma moja nchini humo Bi Farrow amelitaja taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwa nchi yenye watu waliosahaulika zaidi duniani.

Akiyapongeza matamshi ya maafisa wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa balozi huyo mwema ameonya kuwa wanamgambo wanatekeleza dhuluma ambazo zinaweza kutajwa kuwa uhalifu.

Bi Farrow amesema kuwa hakuna sheria kwenye mji mkuuBanguihuku sehemu zingine za nchi zikibaki vijiji vilivyoteketezwa bila watu.

 (Sauti ya Mia FArro) Tafsiri itasomwa huku..

“Si suala lililosahaulika. Ni watu waliosahaulika kabisa. Na ni vigumu kutaka watu kusikiliza janga hili kutokana na hali ilivyo nchini Ufilipino sasa hivi na tukishangaa kuhusu Syria. Lakini watoto kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati pia ni sawa na ninafikiri  tuweza kuwafikia nao pia. Ni eneo lisilo na sheria. Nashindwa kuelewa hili linaelekea wapi. Inaonekana kuwa  hakuna lolote lilioafikwa isipokuwa  watoa huduma za misaada ambao wameamua kujihatarisha kujaribu kuwahudumia watu wanotaabika zaidi duniani, lakini nina matumaini  Umoja wa Mataifa utachukua hatua za kuleta amani”

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa nusu ya watu wote milioni nne wa Jamhuri ya Afrika ya kati wanahitaji misaada ya kibinadamu huku watu 400,000 wakiwa wamekimbia makwao.