Makampuni yalitumia fedha nyingi zaidi kwa kujitangaza:WIPO

14 Novemba 2013

Makampuni kote duniani yanatumia hadi dola nusu trillion kila mwaka kwa kutangaza majina yao zaid ya fedha zinazotumika kwenye utafiti na hata zaidi ya uwekezaji mzima wa kampununi . Alice Kariuki na maelezo kamili.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Hayo yameelezwa kwenye ripoti ya shirika la kimataifa linalohusika na kulinda mali WIPO , ambalo limefanya uchambuzi kuhusu ni jinsi gani makampuni yanaweza kutumia majina kutofautisha bidhaa zao kutoka kwa washindani wao.

Mkurugenzi mkuu wa WIPO Francis Gurry amesema kuwa jina linaonyesha picha nzima ya kampuni na ni moja chombo muhimu zaidi kwa kampuni.

(SAUTI YA FRANCIS GURRY)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo makampuni yaliwekeza dola bilioni 466 kwa majina yao kote duniani mwaka 2011 . Takwimu zote zinaonyesha kuwa matumizi ya sasa kwa ajili ya majina ni dola bilioni 340 mwa 2010 kwa taifa la Mareakani pekee.