Ugonjwa wa Kisukari wakwangua mifuko ya wagonjwa

14 Novemba 2013

Ikiwa siku ya Kisukari duniani hii leo ugonjwa huo umeendelea kuwa tishio kila uchao na sasa inaelezwa kuwa watu Milioni 350 duniani, sawa na asilimia Tano ya wakazi wote wana ugonjwa wa kisukari na idadi inatarajiwa kuongezeka. Ujumbe wa siku hii ni eneza ufahamu kuhusu Kisukari na kinga dhdi yake. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Mitindo ya maisha, kutokuzingatia mlo bora vinatajwa kuchochea idadi ya wagonjwa wa Kisukari. Katika salamu zake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon anataka elimu zaidi juu ya athari za ugonjwa huo na serikali kuweka fursa zaidi kwa watu kuchunguza afya kwani kubaini mapema ugonjwa kunatoa fursa ya kuchukua hatua stahili. Nchini Qatar, ambako Kisukari unazidi kuwa tishio, mtaalamu wa afya Manal Mussalam analaumu aina ya kisasa ya milo akilinganisha na ile ya zamani.

(Sauti ya Manal)

“Awali vyakula ukanda wa Ghuba vilikuwa zaidi ni wali na nyama lakini sasa kuna aina nyingi mno ya vyakula.”

Joseph Abdallah mkazi wa Tanga Tanzania ameishi na ugonjwa wa Kisukari kwa miaka 20 sasa na anasema changamoto ya Kisukari ni zaidi ya ugonjwa kwani…

(Sauti ya Joseph)

Mwaka 2007 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliridhia kuanzishwa kwa siku ya Kisukari tarehe 14 Novemba ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Frederick Banting ambaye yeye na Charles Best, walibuni wazo la kupatikana kwa Insulini mwaka 1922. Insulini ni sehemu ya tiba kwa baadhi ya wagonjwa wa Kisukari.