Tuchukue hatua mapema kudhibiti ugonjwa wa Kisukari: Ban

14 Novemba 2013

Novemba 14 kila mwaka ni siku ya Kisukari duniani ambapo katika salamu zake kwa mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon  amehadharisha juu ya ongezeko la idadi ya wagonjwa hususan watoto, vijana na watu maskini. Amesema takribani watu Milioni 350 duniani waugua Kisukari na licha ya kwamba watu wako hatarini kurithi ugonjwa kwenye ukoo lakini chagizo kikubwa ni mfumo wa maisha ikiwemo kutokufanya mazoezi na milo isiyo na afya. Amesema ni jambo la kustaajabisha katika ulimwengu huu uliosheheni vyakula, bado kuna watu wanashindwa kupata mlo bora. Ametaja hatua za kuchukuakamavile kuwezesha wagonjwa kupata tiba, serikali kuwa na sera za kuhakikisha kilimo na upatikanaji wa vyakula bora na watu kuchunguza afya zao mapema kufahamu iwapo wana Kisukari au la, kwani uchunguzi wa mapema unapunguza madhara makubwa ya kiafya baadaye.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter