Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makosa kwenye mikataba ya awali kuhusu mabadiliko ya tabianchi kuepukwa: Dokta Muyungi

Makosa kwenye mikataba ya awali kuhusu mabadiliko ya tabianchi kuepukwa: Dokta Muyungi

Wataalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi wanaendelea na kikao chao huko Warsaw Poland, matarajio ni kufikiwa makubaliano mapya ifikapo mwaka 2015 kuhusu hali ya hewa kwa mustakhbali endelevu wa dunia, wakati huu ambapo madhara yatokanayo na mabadiliko hayo hayachagui nchi maskini wala tajiri. Dokta Richard Muyungi, ni Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya Kisayansi na Taaluma ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi na akiwa Warsaw alizungumza kwa njia ya simu na Assumpta Massoi wa Idhaa hii kuhusu majaliwa ya kikao hicho ikiwemo mbadala wa biashara ya hewa ya ukaa. Kwanza anaelezea majadiliano yanayoendelea.