Mwaka 2013 watajwa kuwa kati ya miaka yenye joto jingi zaidi duniani

13 Novemba 2013

Mwaka 2013 unaelekea kuwa kati ya miaka kumi iliyo na viwango vya juu zaidi vya joto kuwai kuandikishwa tangu kuanza kunakiliwa kwa takwimu hizo mwaka 1850 kwa mujibu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Kupitia kwa ripoti yake shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO linasema kuwa kuendela kuongezeka kwa joto duniani kunatokana na kuongezeka kwa gesi zinazochafua mazingira ambapo viwango vya vilirekodiwa juu mwka 2012 huku pia viwango vikitarajiwa kuongezeka zaidi mwaka huu.

WMO pia inasema kuwa viwango vya maji ya bahari vimeandikisha rekodi mpya hali ambayo inahatarisha maisha ya wale wanaoishi pwani kutokana na majanga ya kiasili kama vimbunga sawia na janga lilishuhudiwa nchini Ufilipino la kimbunga Haiyan.

Katibu mkuu kwenye shirika la WMO Michel Jarraud anasema kuwa hata kama kupanda kwa joto ni ishara ya mabadiliko ya hali ya hewa athari zake zinaonekana wasi kupitia kwa majanga kama vile ukame na mafuriko.