Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yafanikiwa kufikisha chakula Al Rastan Syria:

WFP yafanikiwa kufikisha chakula Al Rastan Syria:

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP Ijumaa lilifanikiwa kufikisha msafara uliosheheni msaada wa mashirika mbalimbali wa chakula katika eneo la Al Rastan jimbo la Homs nchini Syria. Msaada huo unagawanywa na chama cha msalaba mwekundu cha nchi hiyo .

Msafara huo ulijumuisha malori 9 yaliyokuwa yamebeba vifurishu 5000 vya mgao wa chakula unaotosheleza kulisha watu 25,000 kwa muda wa mwezi mmoja. Wakati wa Oktoba WFP ilipeleka chakula cha kutosha kulisha watu zaidi ya milioni 3.4. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP

 (SAUTI YA ELIZABETH BYRS)