FAO yatoa ombi la dola milioni 24 kugharamia misaada nchini Ufilipino.

12 Novemba 2013

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linakusanya misaada kwa ajili ya waathiriwa wa kimbunga Hayian kilichoikumba Ufilipino na kusababisha uharibifu mkubwa kwa sekta nyingi ikiwemo ya kilimo ambapo pia watu wengi walipoteza maisha.

Mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva amesema kuwa shirika hilo limesimama na kuonyesha uzalendo kwa watu wa Ufilipino. Kimbunga Haiyan kimeacha uharibifu mkubwa na vifo vya maelfu ya watu. Uharibifu ulioshuhudiwa nchini Ufilipino hususan kwenye sekta za uvuvi , kilimo  na misitu unahatarisha maisha na tegemeo la wengi pamoja na usalama wa chakula nchini humo.

Graziano Da Silva amesema kuwa shirika hilo litafanya kila liwezalo kuisaidia serikali ya Ufilipino katika ujenzi mpya likiwa hadi sasa limechangisha dola milioni moja. Naye mkurugeni wa kitengo cha dharura cha FAO Dominique Burgeon anasema kuwa hata kama hakuna picha kamili ya uharibifu kwenye sekta ya kilimo nchini Ufilipino  kuna ushahidi kuwa uharibifu uliopo ni mkubwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter