Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa ombi la dola milioni 300 kuwasaidia waathiriwa wa kimbunga Ufilipino

UM watoa ombi la dola milioni 300 kuwasaidia waathiriwa wa kimbunga Ufilipino

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola milioni 301 zinakazotumika kufadhili misaada ya kibinadamu kwenye maeneo yaliyokumbwa na kimbunga nchini Ufilipino. Karibu watu milioni 11 wameathiriwa na kimbunga hicho huku  watu 700,000 wakilazimika kuhama makwao. Taarifa kamili na Grace Kaneiya

(Taarifa ya  Grace Kaneiya)

Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye maeneo yaliyoathiriwa yanasema kuwa chakula, majisafi, makao na madawa ndivyo vinahitajika kwa dharura.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masula ya kibinadamu (OCHA) linasema kuwa usafiri unasalia kuwa changamoto kubwa kutokana na kuharibika kwa miundo msingi na kufungwa kwa barabara.

Jens Laerke ni msemaji wa OCHA mjiniGeneva.

“Ombi la dola milioni 301 linagharamia kipindi cha miezi sita. Jamii za watoa misaada zinaendela na kupanga oparesheni zake katika kutoa misaada ya kuokoa maisha. Maeneo mengi hayafikiki, tunawafikia hatua kwa hatua. Mahitaji muhimu ni afya, nchakula, madawa, majisafi, usafi na makao. Tumetoa ombi kwa kile tunachokitajakamamawasilano na jamii zilizoathirika, Tunatafuta pia pesa ili kupeleka mawasiliano ya radio kwa kuwa mawasiliano hayapo tena. Pia tunapanga kusambaza radio 1000. Tunaamini mawasiliano ni msaada.”

Shirika la mpango wa  chakula duniani WFP linasema kuwa litahitaji dola milioni 83 kutoa chakula kwa takriban watu milioni 2.5 huku shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNISEF likitoa ombi la dola milioni 34.