Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa Sudan Kusini wajifunza masuala ya uhamiaji nchini Tanzania:IOM

Maafisa wa Sudan Kusini wajifunza masuala ya uhamiaji nchini Tanzania:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekamilisha mafunzo ya siku sita yaliyowaleta maafisa wa uhamiaji kutoka Sudan Kusini hadi nchini Tanzania kujifunza kuhusu njia bora za kudhibiti mipaka na pia kukutana na maafisa wa uhamiaji wa Tanzania. Wawakilishi sita kutoka serikali ya Sudan Kusini idara ya uraia, pasi za kusafiria na uhamiaji (DNPI) akiwemo mkurugenzi wa uhamiaji wameshirikia ziara hiyo ya mafunzo ambayo ilianza novemba 3 na kukamilika Novemba 9. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM

 (SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)