WHO yaonya kuhusu athari na mahitaji ya kiafya Ufilipino

12 Novemba 2013

Shirika la Afya Duniani WHO, limesema linapeleka wataalamu wa afya kwenye maeneo yaloathiriwa na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino ili kusaidia kurejesha huduma za afya.

WHO imesema vituo vingi vya afya viliharibiwa kabisasa, na vile ambavyo vimesalia vimebanwa kwa mahitaji, huku uhaba wa vifaa vya afya ukishuhudiwa.

Tayari matabibu kutoka Ubeljiji, Japan, Israel, na Norway wamepelekwa kwenye maeneo yaloathiriwa vibaya mno ili kuweka vituo vya matibabau vya dharura.

WHO imesema mahitaji ya kiafya ni makubwa mno kwenye maeneo hayo, na huenda hali ikazorota mno kwa sababu za ukosefu wa huduma za usafi na kuchafuliwa maji.

Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO mjini Geneva.

(SAUTI YA TARIK)

WHO imesema tayari pia imepelrka vifaa vya kufanyia upasuaji watu 400, na kukidhi mahitaji ya watu wapatao  120,000 kwa kipindi cha mwezi mmoja.