Kenya, Somalia, UNHCR, zatia saini makubaliano ya wakimbizi

11 Novemba 2013

Serikali ya Kenya na Somalia kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR, leo zimesaini makubali noayeney lengo la kuanzisha msaada wa kisheri ana mingineyo kwa wakimbizi wa Somalia walioo nchini Kenya ambao kwa hiari yao watataka kurejea nchini mwao.

Makubaliano hayo ambayo hayaweki ukomo wa kurejea makwao yanaeleza wajibu wa pande zote tatu kwa mujibu wa sheria za kimataifa kimataifa katika kuhakikisha kwamba hatua ya wakimbizi kurejea makwao ni ya hiari na itafanyika kwa usalama na kujali utu.

Rouf Mazouand ni msemaji wa UNHCR nchini Kenya

(Sauti ya Mazoand)

Wakati hayo yakijiri, naibu Rais wa Kenya William Ruto amewaambia waandishi wa habari kuwa kurudishwa kwa wakimbizi hao kunatokana na sababu za kiusalama

(Sauti ya Ruto)

Kenya ina kambi kubwa ya wakimbizi duniani iitwayo Daadab huku pia kambvi nyingine ya Kakuma ikiwa nchini humo.