Sekta ya afya yakabiliwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi: WHO

11 Novemba 2013

Dunia itakuwa na upungufu wa wafanyakazi milioni 12.9 katika sekta ya afya ifikapo mwaka 2035 huku kwa sasa upungufu huo ukiwa ni milioni 7.2 limesema shirika la afya duniani WHO. WHO inaonya kwamba ikiwa hatua za kuridhisha hazitachukuliwa dhidi ya utafiti huo madahara yake yatakuwa makubwa kwa afaya za mabailioni ya watu duniani kote. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Ripoti hiyo yenye kichwa Ukweli: Hamna afya bila wafanyikazi inaangaza vianzo vya tatizo hilo. Hii ni pamoja na kuzeeka kwa wafanyikazi waliopo sasa, kustaafu au  wafanyikazi wanaohamia kazi za mishahara minono bila ya  wengine kuchukua mahala pao.

Pia kuongezeka kwa mahitaji na idadi ya watu duniani walio na magonjwa sugu kama kisukari. Uhamiaji wa ndani na wa kamataifa kwa wahudumu wa afya vyote hivi vimechangia kuwepo hali hii.

Hata kama ripoti hiyo inazungumzia hatua zilizopigwa kwa mfano mataifa mengi kuongeza wahadumu wa afya wakiwemo wahudumu 23 kwa kila watu 10,000 bado kuna nchi 83 ambazo hazijaafikia hili. Ripoti hiyo inaendela kueleza kuwa siku za baadaye itakuwa vigumu kwa wagonjwa kupata huduma zilizo muhimu. Moja ya hatua zinazostahili kuchukuliwa ni kuhakakikisha kuwa kila mmoja hususan wale wanaoishi vijijini wanapata wahumu wa fya waliohitimu  na wanaofamnya kazi zao vilivyo.