Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wasikatishwe tamaa; washirikisheni kwenye utunzi wa sera: Birungi

Vijana wasikatishwe tamaa; washirikisheni kwenye utunzi wa sera: Birungi

Baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa na kamati ya fedha na uchumi ya Baraza Kuu la umoja huo kwa pamoja wameendesha mkutano kuhusu hatma ya ajira duniani na fursa mwaka 2030 ambapo miongoni mwa mambo yaliyomulikwa ni mustakhabali wa ajira kwa vijana wakati huu ambapo kuna kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia.

Mathalani watoa mada walieleza bayana kuwa kasi hiyo inawezesha kila mtu kuwa mjasiriamali lakini changamoto ni uwezo wa kupata stadi za kuwezesha kujiajiri au kuajiriwa.

Wamesema katika nchi maskini na tajiri bado kuna changamoto ya kuibuka katika mdororo wa kiuchumi ili kuweka fursa ya ajira milioni 470 kati ya mwaka 2015 na 2030 ili kukidhi mahitaji ya idadi ya watu iongezekayo kila uchwao.

Mmoja wa watoa mada ni Barbara Burungi, Mwenyekiti na muasisi wa shirika la Women in Technology kutokaUganda. Yeye anataka mchakato wa kutunga sera usiengue vijana…

(Sauti ya Barbara)

Bi. Birungi akasema vijana waungwe mkono na wapatiwe fursa ya vitendo badala ya nadharia pekee kwani mwelekeo ulivyo wa ukosefu wa stadi kukidhi kasi ya maendeleo utakatisha tamaa vijana kufanya kazi.

(Sauti ya Barbara)