Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia nchini Jamhuri ya Afika ya kati huenda zikafikia hali isiyoweza kudhibitika:PILLAY

Ghasia nchini Jamhuri ya Afika ya kati huenda zikafikia hali isiyoweza kudhibitika:PILLAY

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameonya kuwa uvamizi na ghasia zinazoendelea kushuhudiwa kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati huenda ikalitumbukiza taifa hilo kwenye mzozo mpya . Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 Mnamo tarehe 26 mwezi Oktoba wanamgambo wanaofahamika kama anti-Balaka walivamia na kuteka mji wa Bouar,  mji ulio magharibi mwa nchi kwenye bara bara kuu  ya kwenda nchini Cameroon. Kisa hicho kilisababisha makabiliano makali  ambapo raia 20 waliuawa.  Takriban watu 10,000 wamelazimika kuhama makwao kufuatia mapigano yanayoshuhudiwa ndani na maeno yanayozunguka mji wa Bouar.

Pillay amesema kuwa  Kwa miongo kadha jamii hizo zimeishi pamoja nchini humo akiongeza kuwa chuki iliyopo inastahili kumalizwa kabla  ya haijafikia viwango ambavyo itakuwa vigumu kuzuia.

Pillay amesema kuwa ripoti za hivi majuzi za mauaji ya wanawake na watoto kwenye  kijiji kimoja kilicho mjini Bouar mnamo tarehe 26 mwezi uliopita yanaonyesha viwango vya ghasia zinazoendela kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati na hali ya kutojali ubinadamju. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa

 (SAIUTI YA RUPERT COLVILLE)