Wakati wa kuchukua hatua ni sasa asema Ban akihitimisha ziara Sahel:

8 Novemba 2013

Umewadia wakati wa kuachana na maneno na kuanza kutekeleza kwa vitendo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaambia maafisa wa serikali ya Chad mjini N'Djamena alipokuwa akihitimisha ziara yake katika ukanda wa Sahel kwa mujibu wa André-Michel Essoungou, afisa wa Umoja wa mataifa anayesafiri pamoja na Katibu Mkuu Ban Ki-moon.

Bwana Ban amepokea ushirikiano mkubwa kutoka nchi za Sahel katika mkakati wake wa kulirejesha eneo hilo katika mstari ulionyooka. André-Michel Essoungou anasema mkakati wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sahel unajikita katika nchi tano za ukanda huo ambazo zinamahitaji makubwa ambazo ni Mali, Burkina Fasso, Mauritania, Niger na Chad

 “ Mkakati wa Umoja wa Mataifa Sahel ambao umeandaliwa na timu ya Katibu Mkuu na kupitishwa na baraza la usalama umeungwa mkono kwa kiasi kikubwa katika ukanda mzima kuanzia Mali mwanzo wa ziara hii hadi N'Djamena Chad na tumewasikia mara kadhaa maafisa katika ukanda huu wakisema ni jinsi gani mkakati huu ulivyo fursa muhimu.Na kitu cha muhimu saana ni jinsi wadau wote katika ukanda walivyoipokea ziara hii kama ni ya kipekee". Na sasa tunapaswa kuondoka kwa maneno na kuingia kwenye viotendo, hayo ndio aliyoyasema Katibu Mkuu katika zira nzima hii na hivyo ndivyo anavyotarajia, na wengi watarajie kutokea katika katika wiki na miezi ijayo"