Mkutano wafanyika Hoima, Uganda kuweka mazingira bora kwa wakimbizi: UNHCR

8 Novemba 2013

Hatimaye Shirika la Umoja wa Mataifa kuhudumia wakimbizi la (UNHCR) eneo la magharibi ya kati mwa Uganda, limefanikisha mkutano wa wa wakimbizi wapya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) uliokuwa na lengo la kuleta mshikamano zaidi kati ya serikali ya Uganda, shirika hilo na mashirika mengine ili wakimbizi wapate huduma bora licha ya idadi yao kuongezeka zaidi ya huduma zilizopo kwenye kambi za wakimbizi za Kyangwali na Kiryhandongo.John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, Uganda ana habari kamili.

(Tarifa ya John Kibego)

Kufahamu zaidi kuhusu mkutano huu wa siku mbili unaoendelea mjini Hoima, nimeongea na Alice Litunya Mkuu wa ofisi ya UNHCR ya Hoima.

(Mahojiano na Litunya)

Kambi ya wakimbizi ya Kyangwali pekee imepokea zaidi ya wakimbizi 9,000 kutoka DRC tangu mwezi Julai mwaka huu.