Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua kubwa zilizoikumba Cambodia zaanza kumalizika

Mvua kubwa zilizoikumba Cambodia zaanza kumalizika

Wakati maji yaliyojaa katika majimbo mengi yameaanza kutoweka na msimu wa mvua kuelekea kumalizika, mafuriko mabaya kabisa yaliyoathiri Cambodia tangu mwezi septemba yanaonekana kumalizika limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Kwa mujibu wa shirika hilo mvua kubwa zilisababisha mto Mekong kufurika na kuwaathiri watu zaidi ya milioni 1.7, vikiwemo vifo 188 katika majimbo 20 kati ya 23 ya nchi hiyo. Kufuatia mafuriko hayo watu katika nyumba 31,000 walilazimika kuhamishwa na familia nyingi ndio kwanza zimeanza kurejea katika nyumba zao hivi sasa.