Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu imekaribisha kupiga mweleka kwa kundi la M23 DR Congo:

Ofisi ya haki za binadamu imekaribisha kupiga mweleka kwa kundi la M23 DR Congo:

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa Ijumaa imekaribisha kitendo cha kushindwa kwa kundi la waasi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo kiongozi wa kundi hilo Sultani Makenga ambaye alijisalimisha nchini Uganda ametajwa kuwa ni mmoja wa wakiukaji wakubwa wa haki za binadamu.

Na ofisi hiyo ya haki za binadamu imesema bwana Makenga ni lazima afikiswe kwenye vyombo vya sheria kujibu mashitaka ya ukatili na ukiukaji wa haki za binadamu alioutekeleza.