Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jeshi la DR Congo sasa ladhibiti maeneo yote yaliyokuwa chini ya M23

Jeshi la DR Congo sasa ladhibiti maeneo yote yaliyokuwa chini ya M23

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DR Congo, MONUSCO umethibitisha kuwa jeshi la nchi hiyo hivi sasa linadhibiti maeneo yote ambayo awali yalikuwa chini ya kundi la waasi la M23. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa MONUSCO iliunga mkono hatua za jeshi hilo kwa kutimiza wajibu wake wa kulinda raia.

Amesema Mkuu wa MONUSCO Martin Kobler ametaka kutumia fursa ya sasa kupatia mzozo wa DR Congo suluhu la kisiasa kwa kuendeleza mazungumzo ya Kampala ili hatimaye serikali iweze kupanua wigo wa mamlaka yake na kuleta maendeleo eneohilola nchi. Hata hivyo wametoa angalizo…

(Sauti ya Farhan)

“Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaonya vikundi vingine vya waasi visitumie ombwe la sasa la kusambaratika kwa M2, la sivyo vitachukuliwa hatua na vikosi vya MONUSCO vyenye mamlaka ya kulinda raia.”