Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafi wa Mazingira waangaziwa Nepal

Usafi wa Mazingira waangaziwa Nepal

Muziki unasikika katika sherehe rasmi ilioandaliwa Nepal kwa sababu ya hatua zilizopigwa swala la usafi wa mazingira. Watoto kwa wakubwa wamejumuika pamoja kusherehekea . Hili ni eneo la hivi karibuni zaidi Nepal kutajwa kuzingatia swala la usafi wa mazingira. Hii ni sehemu ya kampeni inayohimiza watu kutumia vyoo na kuzingatia usafi

Hapa tunakutana na mwakilishi wa UNICEF Nepal Hanna Singer:

Ni jambo zuri sana na ni kitu kinachogusa na cha jamii. Ni harakti amabyo imegusa nmioyo na akili za watu wa Nepal na ni kitu ambacho ninafurahi kwa UNICEF inahusishwa nacho.”

Moja ya juhudi za UNICEF ni kushirikiana na shule ili ziweze kuendeleza kampeni hii ambayo imechangia kupungua kwa visa vya kuendesha na watoto wanahudhuria shule.

Wanafunzi wanasaidia kueneza ujumbe kutumia mbinu tofauti kama vile kuzungumza na famila zao na pia kutumia michezo ya kuigiza. Dipish Thapaliya mwenye umri wa miaka 15 yuko katika kamati ya usafi wa mazingira katika shule anakosomea. Ijapokuwa ametoka kwa familia maskini ameweza kuwabadili mtizamo.

Hapa wanafunzi wanaigiza mbele ya wanakijiji kuhusu kijana aliyedungwa na nyoka baada ya kwenda kujisaidia vichakani

Namaste Shrestha ambaye ni mtaalamu wa Usafi, UNICEF Nepal anasema,

Watoto wanajifanyia kazi wenyewe na wanahitaji vyoo nyumbani na vilevile shuleni, programu hii inasaidia kujenga vyoo nyumbani na shuleni. Na watoto wanachukua jukumu la wakala kwani wanafany kazi na wenzao shuleni na jamii zao kwa hivyo ni kama mawakala wa mabadiliko

.Muziki unaendelea , na sherehe inaendelea.