UNFPA yafanikisha ujenzi wa kituo cha elimu ya uzazi Haiti

7 Novemba 2013

Kumeanza kujitokeza hatua ya kutia matumaini nchini Haiti iliyokumbwa na mafuriko makubwa mwaka 2010 ambayo yalivuruga miundo mbinu ikiwemo shule na huduma nyingine za kijamii. 

Tayari Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu limefanikisha ujenzi wa baadhi ya nyumba ikiwemo hospitali na shule jambo ambalo limetoa matumaini makubwa kwa wananchi wa eneo hilo ikiwemo pia wanafunzi. 

Pia UNFPA kwa kushirikiana na taasisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Hait imefanikisha ujenzi wa kituo maalumu ambacho kitatumika kutoa mafunzo ya ukunga na uuguzi .

Zaidi ya wanafunzi 80 wanatazamiwa kupatiwa mafunzo kwa mwaka wa kwanza ikiwa ni hatua za makusudi za kukabiliana na matatizo ya vifo vya kina mama wakati wa kujifungua. Nchi hiyo inatajwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vya kina mama wajawazito duniani.