Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AU yaipongeza Somalia kwa kuanza mazungumzo ya amani

AU yaipongeza Somalia kwa kuanza mazungumzo ya amani

Mwakilishi wa mwenyekiti wa kamishna ya Umoja wa Afrika kwa Somalia balozi Mahamat Saleh Annadif ametuma salama za pongezi kwa serikali ya nchi hiyo na watu wake kwa kufanikisha mkutano wa maridhiano kuhusiana na eneo la Juba.

Balozi Annadif amesema kuwa anamatumaini makubwa kuhusiana na hatua iliyofikiwa na wananchi wa taifa hilo ambao wamedhamiria kupiga hatua juu ya amani.

Mkutano huo wa maridhiano uliofanyika mjini Mogadishu ni sehemu ya utekelezaji wa makubalino ya Addis Ababa yaliyofikiwa Augusti 28 mwaka huu 2013.

Akielezea zaidi kuhusiana na hatua ya kuanza kwa mkutano huo, balozi huyo wa Umoja wa Afrika alisema kuwa jumuiya za kimataifa zitaendelea kuinga mkono Somalia hasa wakati huu inavyopiga hatua kusonga mbele kutekeleza maazimio ya amani.