Muswada wa haki ya faragha kuwasilishwa UM

6 Novemba 2013

Kutoheshimiwa kwa haki ya faragha ndiko kumetusukuma kupeleka muswada wa azimio hili, amesema Christian Doktor ambaye ni msemaji wa ubalozi wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa.

Katika mahojiano na Monica Graylay wa idhaa ya Kireno ya Umoja wa Mataifa Bwana Christaian amesisistiza imani yake juu ya uungwaji mkono kwa azimio hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ujerumani na Brazil. 

Tumetathimni kwamba Haki ya faragha haiheshimiwi katika mawasiliano ya kidijitali na hiyo ndio sababu ya Brazili na Ujerumani zimeamua kuweka juhudi za kupeleka azimio Umoja wa Mataifa ambalo litawezesha ulinzi wa faragha katika ulimwengu wa mawasiliano na dijitali. Mapendekezo tuliyowasilisha kwa wanachama wengine wa UM tayari yameshajadiliwa na sasa yatajadiliwa rasmi katika kamati ya tatu ya baraza kuu ya haki za binadamu na tunaimani kubwa kutokana na mwitikio wa awali kutoka kwa idadi kubwa