Tutumie fursa ya yaliyojiri DR Congo kuleta amani ya kudumu: Baraza la Usalama

6 Novemba 2013

Habari ni njema kutoka DR Congo ambako yathibitishwa kuwa waasi wa M23 wametangaza rasmi kusitisha uasi wao, na hizo ni miongoni mwa taarifa ambazo wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamepatiwa hii leo na Martin Kobler ambaye ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO na mjumbe maalum wa Katibu Mkuu kwa nchi za maziwa makuu Mary Robinson. Kikao hicho kilikuwa cha faragha ambapo Mwakilishi wa kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Gerard Araud akawaeleza waandishi wa habari yaliyojiri kwa muhtasari.  

(Sauti ya Balozi Araud)

Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Novemba, Balozi Liu Jieyi kutokaChinaakasema huu ndio wakati muafaka..

(Sauti ya Balozi Liu)

Baada ya mashauriano  hayo Mwakilishi wa kudumuwa DRCongo, Balozi Atoki Ileka akawaeleza waandishi wa habari kuwa wana furaha kubwa kwa yaliyojiri lakini..

(Sauti ya Balozi Atoki)

“Kama mnavyofahamu sisi hatuwezi kuwa na ushirikiano na majirani zetu iwapo hakuna amani kwenye eneo hilo. Kwa hivyo leo tuna furaha sana kwani adui ameacha uasi. Lakini tunafahamu kuwa kazi bado haijaisha, tutaendelea kuwasaka na kumaliza vikundi vyote vya uasi kwenye eneo hilo la nchi yetu.”

Mwakilishi huyowa DRCongo amesema baada  ya M23 sasa kinachofuatia ni kundi la FDLR ambalo kazi ya kulisaka ilikatizwa baada ya kuibuka kwa M23.